Ijumaa 28 Novemba 2025 - 08:25
Haram Tukufu ya Alawi yapokea Ujumbe wa Iran Unaoshiriki Kwenye Kongamano la Kimataifa la Allama Mirza Na’ini

Hawza/ Katika muktadha wa ushirikiano wa kitamaduni kati ya Iran na Iraq, Haram Tukufu ya Alawi siku ya Jumatano imeupokea ujumbe wa Iran uliokwenda kwenye Kongamano la Mirza Na’ini, ambalo linafanyika  huko Najaf na Karbala.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, katika maandalizi ya kufanyika kwa Kongamano la Pili la Kimataifa la Allama Mirza Na’ini, Haram Tukufu ya Alawi siku ya Jumatano tarehe 5 Azar 1404 Hijria Shamsia, ilikuwa mwenyeji wa ujumbe wa kielimu na kitamaduni uliotumwa kutoka Iran.

Katika hafla hii, Sayyid Isa Kharsan, Mkurugenzi wa Haram ya Alawi, pamoja na wajumbe wa Baraza la Wadhamini, uongozi na wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti na Tafiti za Alawi, pamoja na wahudumu wa vitengo mbalimbali, waliwapokea kwa heshima wageni wa kongamano hili.

Kongamano hili la kimataifa, linaloandaliwa kwa juhudi na ushiriki wa Haram Tukufu za Alawi na Husseini, pamoja na uongozi wa Hawza za Kielimu za Qum, limefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kielimu na kihawza kati ya Iran na Iraq.

Miongoni mwa watu mashuhuri waliopo katika kongamano hili, ni Ayatullah Alireza A’raafi, Mkurugenzi wa Hawza za Kielimu za Iran, ambaye amesafiri kwenda Iraq kwa ajili ya kushiriki katika tukio hili muhimu la kielimu.

Kongamano la Kimataifa la Allama Mirza Na’ini katika awamu yake ya kwanza lilifanyika tarehe 1 Aban 1404 katika mji mtukufu wa Qum, kwa ujumbe wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kwa hotuba maalumu ya Ayatullah al-Udhma Jaafar Subhani, pamoja na kuhudhuriwa na kundi la wanazuoni, walimu na wanafunzi wa Hawza za Kielimu, katika Chuo cha Kiislamu cha Imam Kadhim (a.s). Kisha kongamano hili liliendelea siku ya tatu ya Aban 1404 katika mji mtukufu wa Mashhad. Awamu ya mwisho ya kongamano hili itafanyika katika tarehe 6 na 8 Azar 1404, kwa kufuatana katika miji ya Najaf Ashraf na Karbala tukufu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha